Share:

Serikali yafafanua kufukuzwa nchini bosi wa UNDP

Taarifa iliyotolewa leo April 25 2017 na kitengo cha mawasiliano kwa umma, Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa imesema Serikali imimefikia uamuzi wa kuagiza  Shirika la umoja wa mataifa la Programu ya Maendeleo ‘UNDP’ kumuondoa nchini mkurugenzi wa shirika hilo Awa Dabo kutokana na kutokuwa na maelewano mazuri na baadhi ya watumishi na menejimenti ya shirika hilo.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa kutoelewana kwa mkurugenzi huyo na baadhi ya watendaji kungepelekea kuzorotesha utendaji wa shirika hilo nchini na kupunguza kasi ya kuleta maendeleo kwa Watanzania endapo hatua za haraka zisingechukuliwa.