Share:

Haji Manara asipopata barua yake ya kufungiwa hadi kesho

Mkuu wa Idara ya habari na mawasiliano wa Simba Haji Manara ameonesha dhamira yake ya wazi ya kutaka kukata rufaa ya kupinga kufungiwa mwaka mmoja kujihusisha na soka na faini ya Tsh milioni 9 na TFF na leo April 25 ameandika ujumbe wa kuonesha kwa hamu kusubiri barua ya hukumu yake.

Haji Manara alitangazwa kufungiwa miezi 12 kujihusisha na soka na faini ya Tsh milioni 9 siku ya jumapili ya April 23 lakini bado hajapokea barua “Wasipoleta barua za hukumu zao hadi kesho asubuhi, ntazifuata mwenyewe , tuleteeni barua tuweze kuchukua hatua