Share:

Barakah Da Prince na Naj waivunja internet kwa video ya kikubwa

Barakah Da Prince na Naj wanaendelea kupanda ngazi ya kuwa miongoni mwa couple kwenye burudani zinazo tengeneza vichwa vya habari zaidi.

Na kwa Barakah, huenda ameifahamu vyema ramani ya kutoboa kwenye showbiz kuwa si muziki mzuri tu, bali kuwa na demu mkali na kujiachia naye unavyotaka. 

Jumatatu hii hitmaker huyo wa Siwezi ameonekana kwenye video iliyosambaa Instagram akimmiminia mabusu ya kumwaga mpenzi wake huyo anayeoneka mwenye usingizi mzito.

Bahati ya jitihada za msanii huyo kumwamsha, Naj anaitikia mwito na kubadilisha lips kwa sekunde kadhaa. Video hiyo yenye sekunde takriban 50 imeonekana kuwekwa kwenye account nyingi za Instagram na kuvutia comments za watu wengi wakiwemo waarabu. 

Wawili hao wamekuwa wakifuatana kama kumbi kumbi ikiwa pamoja na kwenda pamoja Afrika Kusini ambako Naj amekuwa akimsaidia mpenzi wake kumtafsiria kwa Kiswahili interview za Kiingereza.